Muimbaji Chris Brown amejikuta aki ‘spend’ weekend yake akiwa katika hali ya wasiwasi baada ya kupata vitisho vya kumuondoa uhai kutoka kwa watu wasiofahamika.
Kwa mujibu wa vyanzo, mwanasheria wa Chris, Mark Geragos alipokea simu kutoka kwa watu tofauti wasiojulikana wakitishia kumuua Chris Brown bila kutoa sababu. Baada ya vitisho hivyo Geragos aliamua kutoa taarifa idara ya polisi ya Los Angeles ambao wanaendelea kufanya upelelezi juu ya vitisho hivyo. Hivi karibuni Chris Brown amekosa maelewano mazuri na majirani zake kutokana na wao kutofurahishwa na graffiti ya Chris aliyoichora nje ya uzio ya nyumba yake ya Hollywood Hills kwa madai kwamba kuna watoto wadogo ambao wanaishi na kupita eneo hilo ambao wanatishika na michoro hiyo yenye muonekano unaotisha, kitu ambacho kinahisiwa kuwa kinaweza kuwa moja ya sababu za vitisho alivyovipata. |
No comments :