technology

business

DIAMOND ALIVYOWAKONGA NYOYO WANANCHI WA IFAKARA

Hiki ndicho kilichonileta haswa mjini Ifakara.....me na team
 yangu nzima ya wasafi kukinukisha
kwenye Mkutano wa C.C.M Kumnadi Mbunge wao anaewania

 nafasi ya Ubunge mjini Ifakara..
kama kawaida yangu sehemu yoyote nafika ili mradi mkono 

uende kinywani kutumia jasho langu
...

Zifuatazo ni Picha Kwenye Nikifanya yangu na Silaha zangu matata 'WASAFI'
Kiukweli tulichelewa kufika kutokana na njia kutokuwa
nzuri,ilitubidi kufika hotelini na kubadilisha
nguo kuvaa magwanda kabisa kwenda kuharibu hali ya hewa
maana naskia kuna nyomi hatariiii.....
Silaha yangu hatari kabisa.....Moses Peter Iyobo in Kesho Song second verse....
Dumi utamu.....wakijikoki kabisa tayari kwenda kufanya
 maangamizi ya kufa mtu....
Afe kipa afe Beki lakini Ushindi Lazima....
Tayari kabisa kuelekea uwanjani kufanya
 maangamizi kama kawaida
yangu mtoto wa kimanyema...
On set camera napenda kuwajuza kila hatua nayo 
kwenda mashabiki zangu kwahiyo
vitu kama hivi lazima viwepo kukujuza wewe 

shabiki wangu wa nguvu...
Umati wa watu ndo ulikuwa hivi kwa nje ya uzio kabla ya
 kufika uwanjani....ilinibidi kushuka
kuelekea uwanjani kwasababu wananchi walizuia njia kwa
shauku ya kuniona....nilikuwa nshachelewa
dakika 10 nyuma.....
Ulinzi ulimarishwa na makadaa na vijana CCM nilipowasili....!!


Unajua mtoto mdogo kama huyu anawaza nini hapo....? ushajuaa bhana....
Shuguli ndo ikaanzia chini sasa kuwaburudisha kidogo kutoa
 ile hali ya fujo na kusukumana
kutokana na umati wa watu,wakubwa kwa wadogo walikuwepo..!!
Baada ya kushtua ngoma moja chini nilienda kuketi
 kwenye jukwaa kuu kusalimiana
na viongozi wa Chama cha Mapinduzi...



Mheshimiwa Getrude Lwakatare alikuwepo pia Kumnadi
Mgombea ubunge huyo kupitia ticketi ya chama cha mapinduzi


Mheshimiwa Samuel Sita akizungumza na wananchi wa Ifakara
 akiwaomba Imani yao juu ya mgombea ubunge wa jimbo ilo....
Mgombea Ubunge wa Ifakara kupitia chama cha mapinduzi
akijinadi kwa wananchi wa jimbo ilo...

Aya sasa baada ya mkutano kumaliza sehemu yake si ndo
mashetani ya kimanyema yalikuwa yamepanda na
si ndo muda ukawa umewadia...ni mpera mpera tu..!!
Huu ndiio umati uliokuwa umefurika mashariki mwa uwanja huu.....
Yaniii.....step by step....''nilikuwaga na mpenzi zamani
akanizngua hvyo nataka mtoto wa Ifakara mimi...




Aghaaa.....kulewa kulewa.....aiyayayayaya kulewa kulewa....
Hahahaha nikiwa stejini uwa ni mwenye furaha usahau
kila kitu nakujiona kama mtoto mchanga asieelewa
yoyote ya walimwengu...


Furaha iliyozidi ilinifanya kushuka chini na kwenda kuwapa
mikono watu walionizidi umri mfano
wa bibi zangu walikuwepo na walinishangaza kufurahia
muziki wangu..hii inanifariji sana
kuona muziki wangu unapendwa na watu wa rika tofauti...

Shangwe iliyoje....kaskazini mwa uwanja huu.....!! I feel Loveeeeeee!!
NIMEMALIZAAAAA.......!!
Baada ya kumaliza show ile jioni ile nilikuwa nimechoka
sana......kilichokuwa akili mwangu ni maji yako wapi
kuweka mwili safiii,kula after that wewe mwenyewe
unajua ni kumcheki mama yangu mama naseeb
kumjulia hali na my baby home....

Emma Platnum baada ya kutoka mzigoni......choka mbaya...!!

Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

3 comments :

  1. kwani ilikuwa ni uchaguzi wa Ubunge au udiwani,nahisi kama umechanganya mkuu.

    ReplyDelete
  2. SAFIIIIIIII SANA SAFIIIIIIIIII SANA INAPENDEZA SANA iFAKARA WALIKUWA WANASIKIA TU.NIMEPENDA WALIIMARISHA SANA ULINZI LA SIVYO USINGEWEZA KUTOKA UWANJANI KILA MMOJA ALITAKA KUKUSHIKA MKONO.ENDELEA KUKAZA BUTI NASUBIRI COMMORO NA TABORA.

    ReplyDelete


three columns

grids

health