Home
/
Slider
/
UJUZI
/
UNATENGENEZAGA CHAPATI KAMA MFUNIKO WA SUFURIA ?NAKUPA SOMO UWE FUNDI WA CHAPATI LAINIII
UNATENGENEZAGA CHAPATI KAMA MFUNIKO WA SUFURIA ?NAKUPA SOMO UWE FUNDI WA CHAPATI LAINIII
Chapati zina ufundi kutoka kukanda, kuzungusha madonge hadi kwenye kuchoma. Ukikosea moja tu baaasssi unatengeneza chapati Ngumu kuliko maisha yako
Unga kg 1 na robo
Chumvi kiasi
Samli vijiko 6 vya kulia......vijaze
Mafuta vijiko 5....
Maji ya baridi (yaliowekwa kwa friji).....
Namna ya kutaarisha.....
Weka unga katika bakuli mimina na chumvi changanya vizur
Pasha moto samli iache ipoe kidogo tu then mimina nusu ya hiyo samli katika unga.... nusu iliobaki weka
Changanya vizuri.....
Weka maji hadi utengeneze donge (usiwe maji mengi sana)....
Kanda hadi iwe laini (hii muhimu kwa ajili ya soft chapati).....
Kata maduara ukuubwa upendano then weka kwa nusu saa ilainike....
Sukuma chapati na weka mafuta 1/2 tablespoon alafu kunja na weka pembeni....
Wacha zilainike.....
Sukuma tena utengeneze duara
Kaanga chapati.....tumia 1 tablespoon kwa kila chapati
Tayar kwa kuliwa
ziada
-maji yanatakiwa yawe ya uvuguvugu kiasi (lukewarm) ama ya ubaridi wa friji kabisa
-kabla ya kuanza kutayarisha chekecha unga (to introduce more air, ambayo ndio haswaa inaumua chapati na kulainisha)
-weka mafuta ya moto sana (kidogo tu) ama weka blue band and rub in (lainisha unga kwa kutumia ncha za vidole tu
-baada ya kukanda, sukuma na kupaka mafuta halafu acha kwa muda kama wa dk 15 hivi. then sukuma kwa kuanza kuchoma.
No comments :