Mwanariadha wa Olimpiki Oscar Pistorius amekutwa na kosa la mauaji baada ya Mahakama ya Afrika Kusini kubadilisha hukumu ya kosa la kuua bila kukusudia.
Oscar alimuua mpenzi wake Reeva Steenkamp Februari 2013 kwa kumfyatulia risasi mara nne kupitia mlango uliofungwa.
Kwa sasa yuko chini ya kifungo cha nyumbani baada ya kutumikia hukumu ya miaka mitano jela.
Pistorius atarudi mahakamani kwa ajili ya hukumu mpya itakayoamuliwa.
No comments :