technology

business

Kikwete awataka Kigoma kutunza barabara, madaraja

RAIS Jakaya Kikwete amewataka wananchi wa mkoa wa Kigoma kuilinda na kuienzi miundombinu ya barabara na madaraja ili idumu kwa muda mrefu na kuhuisha fursa za kiuchumi.
Aliyasema hayo jana mkoani hapa wakati akifungua Daraja la Kikwete na barabara unganishi, miradi iliyogharimu Sh bilioni 90.97.
Daraja hilo lenye jumla ya urefu wa mita 275 katika bonde lenye urefu wa kilomita mbili, limejengwa katika Mto Malagarasi sambamba na ujenzi wa barabara unganishi kwa kiwango cha lami zenye urefu wa kilomita 48.
“Uzinduzi wa daraja hili utafungua fursa mpya ya wakazi wa Kigoma ambapo kabla ya kujengwa kwake hali ilikuwa ni mbaya na wananchi walipoteza maisha… daraja hilo pia limefungua mwelekeo mpya wa uchumi,” alisema.
“Mwaka 2005 wakati napita kuwaomba kura niliahidi nitautazama mkoa wa Kigoma kwa hali ya kipekee na niliahidi kujenga daraja kwenye mto Malagarasi… napata faraja kwamba nimetimiza wajibu wangu na kuwakabidhi daraja hili” alisema.
Aidha, Kikwete aliahidi kwamba barabara ambazo hazijakamilika, watazimalizia na kuishukuru Serikali ya Korea Kusini kwa misaada yake ukiwemo wa daraja hilo.
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

No comments :


three columns

grids

health