Wanasayansi kutoka China waliofanya utafiti
huo wanatumai kuwa utafiti huu unaweza kutumika kuwapa watu
wasio na meno fursa ya kuwa nayo.Wanasayansi
waliofanya utafiti huo, walitumia mkojo wa
binadamu, mwanzoni mwa utafiti wao.Seli zinatokamwilini kwa njia
ya mkojo , zilikusanywa na kuwekwa kwenye mahabara.Mchanganyiko wa
seli hizi na zile zilizokusanywa kutoka kwa panya
ambao hutumiwa kwa utafiti, ziliwekwa ndani ya mwili wa Panya.Baada ya wiki tatu seli hizo zilianza kufanana kama meno zikiwa na sehemu
zote za jino. Hata hivyo meno yenyewe hayakuwa magumu kama meno ya
kawaida.Utafiti huu hata hivyo unahitaji kazi ya
ziada ili kuzalisha meno halisi.Profesa Chris Mason, mwansayansi wa
seli za mwili, alisema kuwa mkojo wa binadamu sio hatua nzuri ya kuanzia
kutengeza meno halisi.Sio kiungo kizuri kutumia kwa sababu mkojo hauna seli nyingi
na kazi ya kugeuza mkojo kuwa seli ni ngumu sana.Pia alionya kuhusu tisho la
maambukizi kutokana na viini vya bakteria vilivyo kwenye mkojo
No comments :