 |
Ukitaja jina la David Luiz kwa kocha wa Chelsea Jose Mourinho basi nadhani ni maumivu ya kichwa yanoyatawala kichwani mwake na akili yote kuznguruka kutafuta dawa ya kuweza kumbakiza beki huyu wa kati mwenye asili ya kibrazil kwa wazee wa ''The Blues''
Lakini Hali inaonekana kuwa ngumu kila kukicha baada ya timu kama Barcelona kuonesha nia ya kumsajiuli beki huyu licha ya kuwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya chelsea ya Uingereza... Katika mazungumzo na waandishi wa habari akijibu swali la mwandishi wa habari kutoonekana kwa David mazoezini alikuwa na haya ya kusema ''Bado nazungumza na kijana wangu,napenda kumuona akizidi kuwepo nasi hapa na yupo kwenye mikakati yangu ya kugombea ubingwa wa vikombe vingi nikiwa hapa darajani''
Alizidi kufunguka juu ya Kupokea Ofa toka kwa Barcelona alikuwa na haya ya kusema ''Unajua aikatazwi kwa timu yoyote kupendezwa na mchezaji yoyote lakini lazima sheria zifatwe lakini licha ya hivyo sisi kama timu atuna mpango wa kumuuza David kwa timu yoyote,tupo nae mezani kushugulikia maswala yake ya mkataba mpya na ni maswala kadhaa tu yanamaliziwa na hali itakuwa shwari'' Alisema Kocha huyo anaejulikana kwa jina la 'The Special One'
Habari za ndani zimeweza patikanika ni kwamba David Luiz amezidi kuwachanganya uongozi wa Chelsea baada ya kugomea kusaini mkataba mpya na kinachosemekana ni kwamba anaona kama ni dharau yeye kucheleweshewa kupewa mkataba mpya kilabuni hapo so aina budi yeye kuangalia njia nyingine ya kujinufaisha zaidi.
Swala hili ndilo lazidi kumchanganya Kocha Jose Mourinho kwa hali zaidi..... Tusubiri tuone kitakachojiri mwishoni mwa dirisha la usajili litakavyofungwa mnamo tarehe 31.8.2013....Je David Luiz atabakia Chelsea au Kutimkia Barcelona....?
Usikose kupitia Blogsite yako hii ya Kijanja zaidi kupata Updates za uhakika zaidi... |
Ebu otea David Luiz atachezea timu gani kabla ya dirisha la uchaguzi alijafungwa....?
No comments :