Drake,mwanamuziki mwenye asili ya canada au waeza muita member wa Young Money,Label
inayofanya vizuri duniani kwenye kila idara anatazamiwa kuachia Album yake mpya hivi karibuni. Album hiyo inayoenda kwa jina la''NOTHING WAS THE SAME,inatarajiwa kuachiwa jijini New York September mwaka huu. Drake akionekana mwenye furaha alifunguka pia juu ya ujio wake wa Album hiyo huku akimshukru Mwenyezi Mungu na kutoa Ufafanuzi juu ya Cover ya Album yake, alikuwa na haya yakusema ''Kwanza namshukru Mungu,ananipigania kwenye kazi yangu...Ujio wa Album hii nimejipanga zaidi kuleta mabadiliko kwenye muziki wa nchi yangu na kuwafumba midomo watoto wadogo waliotukuta kwenye gemu'' Aidha alizidi kumshukru Mchoraji Kadir Nelson toka Marekani kwa kubuni cover hiyo inayoonekana hapo juu. ''Cover imetulia,nimeipenda,imebeba ujumbe wote wa Album kama jian lenyewe unavyolisikia.
Ebhana eeeh hii balaa Mnyamwezi Drake anajipanga kuachia kitu Soon so kama wewe ni shabiki wa Drake kaa mkao wa kura,24th September mzigo kuachiwa. |
No comments :