Jeshi la polisi la Tanzania kupitia kamanda wa kanda ya Dar es salaam wametoa donge nono la Milioni 100 za kitanzania kwa atakaefanikisha
kukamatwa kwa watu waliosababisha kuunguzwa kwa waingereza wawili kisiwani zanzibar wikii moja iliyopita... Akizungumza kamanda Kova alisema ''Jeshi la polisi limetoa milioni 100 kwa mtu yoyote atakaesaidia jeshi ili kuweza kumpata mtu mwenye mtandao huo wa kinyama cha kuwajeruhi watu kwa kutumia tindikali...,basi milioni 100 hizi zitakuwa za kwake....''
Jeshi la polisi limetoa kiasi hiko kama changamoto kwa wananchi wa Tanzania nzima kuweza kulisaidia jeshi la polisi kwenye msako huo ambao kwa sasa kupitia tukio ilo limeweza kuichafua nchi kwa kiasi kikubwa kwenye maswala ya kiusalama kwa wageni na hata watali kuanza kuofia hali yao ya usalama.....
Jambo ili limetokea wikii mbili baada ya mmiliki wa Home shopping centre na msasani city mall kumwagiwa tindikali na mtu asiejulikana jiji dar es salaam lakini ili limetokea kisiwani zanzibar kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 kumwagiwa tindikali na watu wasiowajua wakiwa kisiwani hapa kwa maswala ya ufundishaji watoto yatima..... |
No comments :