technology

business

NEWS:IRENE PAUL ADAIWA KUFICHA UJAUZITO WAKE

Actress maarufu nchini Irene Paul anadaiwa kuwa
mjamzito lakini mwenyewe anadaiwa kuficha watu
wakiwemo mapaparazi ili wasijue kuwa
tayari kanasa. Inadaiwa star huyo anayetamba na
 filamu kibao ana dalili zote za ujauzito kwa mujibu wa
 chanzo kimoja kilicho karibu nae lakini haijulikani
kwanini hataki kuweka wazi hata kwa watu wake
 wa karibu. "sijajua kwanini hataki watu wajue kama
ana ujauzito labda anataka watu washtukie tu
amejifungua mtoto. Lakini ajue yeye ni star hata
 afanyeje hawezi kulificha tumbo lake litakapokuwa
kubwa" kilisema chanzo hicho kikizungumza na mtandao mmoja.


Baada ya kupata habari hizo ilibidi Thisisdiamond imtafute Irene Paul ili kusikia upande wake kama
 kweli ni mjamzito au lah lakini mpaka tunaandika
habari hii muigizaji huyo hakutoa ushirikiano wowote ule.

Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

No comments :


three columns

grids

health