Huddah Monroe a.k.a Boss Lady wa kenya, alikuwa mwakilishi wa Kenya kwenye Big Brother mwaka huu lakini bahati aikuwa kwake mapema aling'atuka kwenye Jumba ilo..... Juzi kati alipost kwenye mtandao wake wa Twitter kuwajuza mashabiki zake kuwa atokuwepo kwenye finali za Big Brother mwaka huu kutokana na majukumu na mambo kuingiliana hadi kufikia kushindwa kuyatatua kwa muda muafaka so atokuwepo..... Kilichojiri hapo ni mashabiki zake kuanza kulalama kiasi kwamba wengine kutukana,
Lakini Suprise iliyoje....??? Huddah majira ya usiku wa jana Ali tweet kwenye mtandao wake wa Twitter na kuandika yupo Airport kuelekea Nchini S.A kwenye Finali hizo zinazofanyika siku ya leo.
Inavyoonekana Boss Lady huyu ameshatatua matatizo yake sasa yupo njiani kuelekea nchini S.A lakini kwa upade mwingine naweza sema labda Huddah alikuwa anatingisha kiberiti kuona umuhimu wake kwa mashabiki zake.........
Tusubiri tujione kitakachojiri kwenye Finali hizo nchini South Africa. |
No comments :