technology

business

NEWS:HIVI NDIVYO NILIVYOSHUHUDIA AIRPORT YA NAIROBI IKIWAKA MOTO NIKIWA NJIANI KURUDI BONGO

Hapa unapo paona ndo hali ilivyokuwa majira ya saa 1 asubuhii ndani ya Nairobi....
Niliwasili Alfajiri ya saa kumi na moja nikitokea nchini South Africa
nilikuwa napita kubadilisha ndege kurejea nyumbani Bongo Lakini
maswahibu haya yaliyotokea majira ya saa 1 asubuhi huku mimi
na abiria wengine tukisubiri  kwenye ndege ghafla tulikuja kujuzwa kuwa hali ya
usalama pale Airport haikuwa shwari na tulivyotoka kwenye ndege
ndio niliposhudia uwanja wa ndege wa Kenya ukiwaka moto....
Hadi sasa sasa chanzo cha moto ule uliosababisha kuwaka kwa Airport bado sijajua lakini
hii imepelekea safari kukwama,sina uhakika kama tutaweza kuja Dar  tena au Ndege
kama zitaweza kuruka kwa leo maana hapa tulipo wanatupeleka hotelini,
Imewalazimu Uongozi wa Immigration kuja na kutugonga mihuri kwenye basi
la wasafiri na kuwekewa usalama wa mabegi yetu....

Zifuatazo ni Picha za Tukio zima Pale Airport ya Nairobi.....!!

Abiria wote wakiwa wanaamishwa kuelekea Hotelini......

Choka sana nishapamiss Bongo alafu haya ndo yanatokea nipo
na mwanangu Moses Iyobo kuelekea Hotelini maana bado sijapata
uhakika wa safari...








Baada kama ya Lisaa hivi ya kukaa kwenye bus wameamua kutuleta hoteli maeneo ya huku huku
Nairobi,Hoteli hii Inaitwa Panari(5star hotel)


Mabegi yakiwa yamewekwa kwenye hali ya usalama kabisa.....





Kiukweli ni jambo la kumshukuru Mungu kwangu mimi na Abiria
 wote kutuepushia na mabalaa  yoyote
tangu mwanzo wa safari hadi hapa tulipo na Mwenyezi Mungu
akasimame nasi kutufikisha nyumbani salama...
Kaa nami kwenye Blogsite yako ya kijanja zaidi ntazidi
kukujuza kinachojiri huku
na kujua chanzo cha moto huu.....


Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

4 comments :

  1. Poleni kwa yote. Lakini langu ni swali mmoja, mbili. Fununu ni kwamba mwaja Kenya friday usiku KICC na sunday Mombasa beach, Is this true and tickest zauzwa wapi n how much?

    ReplyDelete
  2. pole sana Diamond ,mimi ndiyo kwanza baada ya kuingia kwenye blog hii ndiyo napata taarifa mwenyezi Mungu amekunusuru,na ataendelea kukunusuru na yale yote mabaya dua twakuombea kila siku naona mfungu unakwisha tunasubiri nyimbo mpya kwa hamu kubwa

    ReplyDelete


three columns

grids

health