Imekuwa kawaida kwa wanamuziki wengi duniani baada ya mafanikio kwenye muziki ukaa chini
na kurudisha shukrani kwa mashabiki zao kutokana na wao kununua kazi zao na kuwafanya wafike hapo walipo kiuchumi na hata kimaendeleo pia...
Hali hii pia imetokea kwa mwanamuziko toka Nigeria anaefahamika kama Davido,siku ya jana aliweka bayana kwenye mtandao wake wa kijamii kuwa ana mategemeo ya kujenga shule na yupo kwenye mikakati bado ya kununua ardhi ili aweze kuanza utaratibu huo..... Na alizidi weka wazi kuwa ataanzia kwenye jimbo la Osun nchini Nigeria na kuzidi kusogea kwenye miji mingine kutimiza azma yake ya kujenga shule kwaajili ya jamii.......
Inavyoonekana jamaa ana mpunga mrefu sana na ana moyo wa kusaidia,inapendeza sana kwa kikubwa au kidogo ulichonacho kugawana na wasiojiweza, Mungu azidi kumbariki Davido....
Unaweza kucheki chini hapa kuona kile nachokuambia pale msanii huyu alipo tweet kwenye mtandao wake huo wa kijamii..... |
No comments :