Namshukuru Mungu Baada ya kukwama juzi nikiwa safarini nchini Kenya,nikitokea nchini South Africa baada ya Airport nchini humo kuungua kwa Moto,jana majira ya usiku
niliweza wasili salama salimini kabisa kwa uwezo wa Allah,lakini Shukrani za Pekee ziwaende Coca-Cola walitisha sana pale kuona tunachelewa fanya Tangazo kwenye ratiba waliamua kukodi ndege maalumu iliyoweza kunifikisha usiku wa jana on time na kuanza kujipanga ili kuweza kufanikisha mpango mzima wa Tangazo la kinywaji cha Coca-Cola. Kinywaji Murua popote uendapo, utakapo kuwepo na marafiki ata wakati wa kupata msosi mezani coca-cola inakufaha zaidi....
Siku ya Leo ndio nilikuwa kwenye michakato kama Balozi wa Coca-Cola Tanzania kuweza kufanya tangazo maalum kwaajili ya Bidhaa ya kampuni yetu nchini Tanzania na duniani kiujumla......Nimeshoot tangazo ili nikionekana natembea nikinywa kinywaji hiki kizuri zaidi duniani...
Nimechoka sana muda huu baada ya kuwa busy siku nzima ebu tizama picha hizi mbili nilzokuwekea mtu wangu wa kweli alafu mapicha picha zaidi yanakuja muda si muda. Nawapenda sana,Jioni Njema.... |
I love Tanzanian Swahili, just sounds funny. Ati 'michakato''msosi' eih yawa...
ReplyDeletepole na misikosuko ya uwanjani tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukunusuru na kurejea nyumbani salama na kuendelea na kazi kama balozi wetu ukawakilisha
ReplyDeleteU shine bro. Keep it tight now coz kuna kupanda na kushuka
ReplyDelete