Inafurahisha ila kwa upande mwingine inastahajabisha....Kweli hela ukiwa nayo basi utataka kufanya jambo lolote uliwezalo ukijua hela yaweza fanya....
Msanii aliechipukia kwenye miaka ya 2011 Hapa namzungumzia Justin Bieber msanii aliezinduliwa kipaji chake na Msanii Usher Raymiond kupitia videoz za Youtube.... Hiki kimbwanga alichokifanya ni baada ya kutumia dola laki moja kubadilisha rangi ya gari lake Audi kuwa na rangi ya Leopard, kwa kiswahili mnyama huyo anaitwa Duma..... Amebadilisha rangi hiyo sasa yapata muda wa week 2 sasa kwa gharama za pesa za kitanzania milioni mia moja na 32 kwa hesabu za haraka...... Sasa unaweza kuona ni kitu kwake kidogo lakini kisu hicho kirefu kibongo bongo ni mradi tosha kwa mfanyabiashara wa aina yoyote japo kwake msanii huyo anaona ni kitu cha kawaida cha kufurahisha nafsi.... |
No comments :