Kwa sasa ukizungumzia jina ili Hasheem Thabeet, kwenye ligi kuu ya kikapu nchini Marekani basi autoacha kusikia jina kila mmoja akimzungumzia....Mtanzania Pekee kwenye Ligi ya kikapu maarufu na nguli ulimwenguni ijulikanayo kama NBA....!! Kwanini Hasheem......?? Basi kama ulikuwa hujui acha nkujuze mimi leo,Hasheem kwa sasa ndie mchezaji mrefu kuliko wote kwenye Ligi hiyo ya kikapu marekani iliyojawa na Mastaa nguli Duniani kwenye timu tofauti tofauti.... Mtanzania huyo mwenye urefu wa Futi 7.3 ameweza kuweka Historia hiyo baada ya aliekuwa anaongoza kwa kipindi kirefu,mchezaji kikapu mwenzie Yao-Ming kusataafu kucheza kikapu mwanzoni mwa mwaka huu... Hasheem Thabeet anaechezea Timu ya Oklahoma City Thunder hadi sasa aijaonekana mchezaji yoyote kumkaribia mchezaji huyo kwa karibu zaidi ya Mchezaji Dwight Howard anaecheza ligii hiyo....!! Hasheem Thabeet aliezaliwa february 16 mwaka 1987 nchini Tanzania na kukulia jijini Dar es salaam kabla ya kwenda nchini marekani kimasomo mwaka 2006 na hadi kufikia mwaka 2009 kupata nafasi kucheza NBA... Hasheem anaechezea Oklahoma City Thunder anapokea kiasi cha dola za kimarekani 6.128 milioni kwa mwaka baada ya makato ya kodi nchini humo.....!!
Big Up kwa Hasheem Thabeet anavyozidi kuitangaza Bendera ya Tanzania na East Africa nzima kwenye Ligi hiyo Kubwa duniani... |
No comments :