Kama utakuwa na kumbukumbu basi moja ya makala ambazo nimekuandalia huu ni mwendelezo wake... Makala ya Jinsi Dubai ilivyokuwa hadi leo walivyowekeza na vitega uchumi,nikiwa nimekuonesha sehemu mojawapo za vitega uchumi vya nchi hii ya falme za kiarabu...... Picha hizi utakazoziona hapa ni picha halisia za maendeleo ya nchi hiyo mojawapo unaweza kujionea jinsi mfano wa Mti wa Mnazi na Matawi yake lakini hapa unajionea mti huo ukiwekwa baharini ukitengenezwa kwa kusukuma maji na kujenga makazi ya watu na hoteli za kitalii.. Kama ulikuwa hujui basi acha nikujuze hapa,kwa sasa Dubai ndio Mji mzuri kupita miji yoyote duniani kutokana na vitega uchumi kama hivi,ni ajabu kuona au kufikiria kufanya kitu kama hiki,cha kwanza yahitaji moyo cha pili yahitaji ushirikiano na moja ya hela zilizotumika ni kodi za wananchi na hela ya serikali.... Hii inatokanaje.......? Je wajua?? Serikali yenye watendaji Imara na Uadilifu wanaweza kufanikisha mambo kama haya kuzuia ufujaji wa hela na rushwa huku Dubai rushwa ni adui namba moja na kutokana na sheria ya nchini humo ukipokea rushwa ni kuhukumiwa kunyongwa........ Hali kama hiyo inatisha hadi viongozi na kuamua kujitolea kufanya kazi kwa hali na mali kufikia kuwaletea maendeleo wananchi wake..... |
No comments :