Hii ni habari njema kwa Nisha's Film Production na kwa soko zima la sanaa ya Bongo movie.... Hii imetolewa na wasambazaji nguli na maarufu nchini Tanzania Steps Entertainment kuwa Movie ya TIKISA iliyofanywa chini ya kampuni ya mwanadada mjasiriamali na mwenye kiu ya mafanikio yani hapa namzungumzia Nisha Bebe Pusi ndio filamu iliyoleta faida tele ndani ya Mwezi wa 6 na wa 7 kwenye kampuni hiyo..... Aidha Steps aikuweka wazi ni kiwango gani au kiasi cha pesa walichoingiza lakini wamesema wanafurahishwa sana kuona mapato yale tofauti na walivyotegemea msemaji wa Steps akiongea''Tunafurahi kuona kwenye sanaa ya filamu mwanamke anafanya vizuri kwenye mauzo uku tushazoea movie za wanaume wakiwashirikisha wanawake kufanya vizuri,lakini hii imedhihirisha vingine kabisa....inatupa moyo kuendelea kufanya nae kazi sababu ni mtu ambae anajua anachokifanya na anapenda anachokifanya'' Alizungumza msemaji wa Steps Entertainment.... Kwa upande wa wanawake kwa sasa inaonekana wanakuja juu kwenye mapinduzi ya filamu Bongo... Haya Kila kheri kwa mwanadada Nisha na Production nzima na pongezi kwa kufanya kitu kizuri kwenye sanaa ya Bongo Movie...!! |
Nisha ni mzuri nakubaliana na hilo kwenye Matrida na red cross ulizitendea haki hizi filam kiukweli ni nzuri na napenda kukuangalia unavyo act sisi wadau wa Diamond tunakutakia baraka tele zitokazo kwake mwenyezi mungu na zikuendee hata katika shughuli zako kwa ujumla.mfuatilie sana mtitu game quality utafika mbali.tunashukuru kwa kutujuza This is Diamond maana bila ya wewe wengine tusingejua niwatakie swaumu njema
ReplyDelete