Kwa sasa hii ndio habari moto moto ukizungumzia muziki duniani..... Msanii Jay-Z baada ya Album yake kuachiwa sasa yapata siku 8 na imefanya vizuri kupita ile album yake ya miaka 2 nyuma....
'MAGNUM CARTA HOLLY GRAIL'' Ndio jina la Album Hiyo..... Maana halisi ya jina hilo ni ''Kuhusiana na utawala wa kiingereza na watu wake baada ya kupumzika kwa muda sasa ikawa ni muda wa kufanya kazi kutengeneza hela... hii ikimaanisha baada ya Jay-z kukaa kipindi kirefu sasa ni muda wa kutengeneza hela.... Album hiyo imefanya vizuri sana kupita album zote zilizotolewa ndani ya miezi 3 nyuma hapa nikimaanisha kuanzia mwezi wa 3 hadi sasa 7.... Baadhi ya wadau wanasema album hiyo imepata promo kubwa kutokana na mkataba wa Jay-Z na kampuni ya simu ya Samsung kumpa donge nono kuwauzia robo tatu ya hisa za album hiyo,japokuwa hadi sasa ni asilimia 14.3 ya watumiaji wa Samsung Android walioweza kuipata Album hiyo kutoka kwenye mtandao kwa bei chee.......huku Album hiyo ikisimamiwa na Sony kwenye usambazaji wake.... Ukiachanana hayo Album hiyo pia imepata promo kubwa kutoka vituo vya Televison na hata kwenye mitandao mikubwa ikiwemo hata kutoka kwa wasanii wakubwa kama Usher Raymond,Justin Timberlake, Producer Timberland,Pherrel williams,Chris Brown,Swizz Beatz na Snoop Lion.... Hiyo pia ndio sababu muhimu ya album hiyo kufanya vizuri ndani ya week moja na siku moja.... |
No comments :