technology

business

JAY-Z ALAMBA DILI NONO KUTOKA SAMSUNG..

Rapper Jay-z kutoka Marekani amelamba dili nono kutoka kampuni
 ya simu Samsung aliweka wazi usiku wa jana

...
Jay-z akionekana kwenye video Promotion aliyofanya ya dakika 3
akiwa studio,ikiwataharifu mashabiki zake duniani
kote kuwa ''Kila mwenye simu ya aina ya Samsung Galaxy ataweza
 kupata Album yake Mpya inayoenda kwa jina
la''MAGNA CARTA HOLY GRAIL'' ambayo ameizindua cover
ya Album jumapili ya Juzi wakati wa mechi ya kikapu
kati Miami Heat vs San Antonio Spurs nchini Marekani.......

Watumiaji wa Samsung Galaxy wataweza kupata Album hiyo
kupitia Application itakayokuwepo kwenye simu hiyo
kuanzia July Mosi,hiyo itakuwa baada ya siku tatu Jay-z
 kuiachia Album yake hiyo....
 Video hiyo ya Promo kuweka uhakika zaidi akifanyia kazi album
yake hiyo inamwonesha akiwa studio na
producer Timbaland,mwanamuziki Swizz Beats na Pharrell
williams wakimalizia matayarisho ya album hiyo...

Samsung wameweza kununua copy Milioni Moja za Album hiyo
mahususi kwaajili ya watumiaji wa Samsung Galaxy
kwa kiasi cha dollar za kimarekani Milioni 5 kwa pesa za
kitanzania ni zaidi ya Bilioni 7.2...
 Katika kuleta ukaribu na Jay-z na Samsung waliweza pia kuingia
 nae ubia wa mwaka mmoja kutangaza Simu zao
Galaxy tu kwa kitita cha dolla za kimarekani milioni $20 zaidi ya
 bilioni 36 za kitanzania.....
Hii inatokana na mashindano ya kibiashara zaidi kutokana na
Samsung kuonekana kushindana kwenye
biashara na Kampuni ya simu za Apple wanaotengeneza
 simu za Iphone na Brand nyingine za Mitandao....

Hii inakuwa sawa na Msanii Beyonce mkewe na Jay-Z
alivyosaini mkataba na pepsi,kama mwanamuzii wa kike
Alicia keys alivyosaini mkataba  kampuni ya simu za
Smartphone Blackberry
na wengine wengineo...!!

All the best kwa Jay-Z hii naonesha ni jinsi gani muziki wao
unathaminiwa kutokana na kazi zao nzuri kuweza kupata
mikataba minono....!!


Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

No comments :


three columns

grids

health