technology

business

MAELFU KWA MAELFU WAMZIKA BI KIDUDE KISIWANI ZANZIBAR

Jana alasiri ilikuwa safari ya mwisho kwa Bi kidude baada ya kumaliza
swala na kumpumzisha
kwenye makazi yake ya milele......maelfu ya wananchi wakubwa
kwa watoto walifurika sana
kwenye mazishi ya kikongwe huyu alietutoka ghafla 17april majira
ya saa 7 mchana kwa saa za afrika
ya mashariki.....Viongozi wengi wa nchini walijumuika na familia
katika maziko ya Bi kidude pamoja hata na
wasanii pia walikuwepo kuonesha mchango wao.....

Zifuatazo ni picha wakati maiti ikiswaliwa Mskitini na safari ya kuelekea makaburini kwa maziko

Mwenyekito wa baraza la mapinduzi zanzibar Dk
Mohamed Shein akiwasili msikitini kwaajil ya swala
ya kuombea maiti....

Mwili wa marehemu Bi Kidude ukitolewa nje ya mskiti tayari kabisa kwa kuelekea
makaburini....baada ya kumaliza kuswaliwa








Licha ya mvua kali lakini watu walihakikisha mpaka
 mwili uingie kaburini na tufukie ndo
mengine yatafata....

Ulinzi ulihimarika sana maeneo haya.......

Viongozi wanchi wakiwasili makaburini tayari kabisa kwa maziko
Rais wa Jamhuri ya mungano wa Tanzania Dk Jakaya na
Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi ndugu
Ali Mohamed Shein wakiwasili makaburini kwa ajili ya maziko
Rais Jakya alihairisha ziara yake ya nchini Uholanzi na kurudi kuja kumzika
legendary wa Tanzania,Fatuma binti Baraka.....


Issa Michuzi nae alikuwepo kuhakikisha akosi matukio kwa ajili ya habari za mitandao


Diamond pia alikuwepo bega kwa bega mpaka mwisho
 wa maziko bila kujali mvua....na hali
ya matope iliyokuwepo wakati huo
Licha ya kuwa na Mvua Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa
Tanzania Dk.Jakaya mrisho kikwete
na Mwenyekit wa Baraza la mapinduzi Dk Muhamed Shein
walikuwepo makaburini mpaka mwisho
wa maziko....!!

 

Boss Ruge wa Clouds Media akiwa tapa tapa makaburini baada ya mvua kubwa kunyesha
Mwana Fa  na Fid Q baada ya maziko........awakujali mvua
...kuwanyeshea ...lakini bibi aende salama..
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

1 comment :

  1. polen sana bro, huo ndo ubnadamu wa kweli, thanx kwa kutujuza mambo yalivyokwenda huko

    ReplyDelete


three columns

grids

health