Bibi Atupele pembeni akiwa na Mjukuu wake kwenye picha ya Pamoja...Bibi huyo anaedhaniwa Mchawi Baada ya vitendo vya kichawi kukithiri kijijini hapo.... Ni Baada ya Mtoto wa Miaka 11 kupotea Ghafla baada tu ya kuena kumsalimia Bibi huyo Nyumbani kwake Majira ya Ya Saa 11 Jioni.....!! Bibi Huyo mwenye Umri wa Miaka (60) aishie kata ya masewe wilayani Ilemi Mkoani Mbeya...Jana alinusurika kifo Baada ya wananchi wenye Hasira kali kuchoshwa na Vitendo vya Kichawi vinavyoendelea kijijini hapo na vyoye Bibi huyo akiusishwa..
Walisema katika vikao kadhaa vilivyoitishwa mtaani hapo kwa ajili ya kutafuta mbinu za kupatikana kwa mtoto lakini Mwanamke huyo hakuonesha ushirikiano jambo ambalo lilizua hofu miongoni mwa wakazi hao hali iliyopelekea kuhisiwa kuhusika na tukio hilo. Walisema katika kikao kilichofanyika Machi 23 Mwaka huu majira ya Asubuhi mtaani hapo wananchi hao waliendelea kusisitiza kuwa Mwanamke huyo achukuliwe hatua kwa kuwa ndiye anayehusika na upotevu wa motto ambapo iliamriwa kwenda nyumbani kwake kufanya upekuzi. Walisema baada ya kufika nyumbani kwake na kufanya upekuzi walikuta vitu vinavyohisiwa kuwa vinahusika na ushirikina ambavyo ni vitovu vya watoto wachanga watatu ambapo Mwanamke huyo baada ya kuulizwa alishindwa kutolea ufafanuzi hali iliyosababisha wananchi kupandwa na hasira na kuanza kumpiga. Kutokana na tukio hilo Kaimu Mwenyekiti wa Mtaa huo Nedy Mwamlima alimnusuru Mwanamke huyo katika kipigo kutoka kwa wananchi kwa kumpeleka katika kituo kikuu cha Polisi kwa usalama zaidi. Baada ya mtuhumiwa huyo kunusuriwa na kukimbizwa katika kituo cha Polisi wananchi hao hawakupoza jazba zao ambapo waliamua kuteketeza nyumba ya mtuhumiwa ikiwa ni pamoja na kufyeka mazao yaliyokuwa yamepandwa jirani na nyumba yake. Hata hivyo hasira za wananchi hao hazikuishia hapo bali walimsakama Mwanamke mwingine aliyejulikana kwa jina la Agnes Sika ambaye ni mke wa Mchungaji wa kanisa la Pentecost Groly kwa madai kuwa ni rafiki wa mtuhumiwa na amekuwa akimfichia siri. Jeshi la Polisi liliwahi kufika eneo laTukio na kumnusuru Agnes asipatwe na madhara ikiwa ni pamoja na kutochomewa nyumba yake ambayo tayari wananchi hao walionekana kuikimbilia kwa ajili ya kutaka kuibomoa. Aidha Jeshi la polisi linaendelea kumshikilia mtuhumiwa kwa ajili ya mahojiano zaidi pamoja na upelezi ambapo Baba mzazi wa Mtoto anayesadikiwa kupotea katika Mazingira ya kutatanisha akisema anamwachia Mungu baada ya juhudi za kumtafuta kushindikana.
|
Daaahhh nimehisi kama ni mimi niliye fanyiwa kitendo hicho cha kinyama kumbuka ana watoto sasa watoto hawana makosa yoyote ata kama nyanya yao ni mshirikina lakini watoto hawahusiki kabisa sasa angalia watoto watalala wapi malaika wa Mungu...??? so sad imeniuma sana
ReplyDeleteyani ww jackson ulivonichefua na maneno yako, yani ww unawafikilia watoto sijui wajukuu wa uyo bibi watalala wapi. mbona humfikilii mtoto wa binadamu mwenzako aliyepotea kwenye mazingila ya kutatanisha yupo hai au wameshamuuua.wakati inaonekana wazi uyo bibi ameusika, kama yeye sio mwanga ivyo vitovu alivyokutwa navyo kavipata wapi na vinafanya nini kwake?
ReplyDelete