technology

business

TANZANIA YACHUKUA NAFASI YA KUMI NDANI YA LONDON FASHION WEEK..!

Wanamitindo wa Kitanzania- Anna Lukindo, Christine Mhando na Jacqueline Kibacha
Jumapili mchana wilaya ya Westminster jijini London ilikuwa na
 mashindano
 ya ubunifu na urembo katika maonyesho ya kimataifa ya
London Fashion Week 
 Mashindano haya yalifanyika jumba
. la Somerset lililosimama imara kwenye
 upembe wa kaskazi ya mto Thames.
Anna Luks
Mshindi wa tukio alikua Estonia. Ingawa Tanzania haikuwa mshindi wa mwanzo-
 ilichaguliwa kati ya
 Kumi Bora jambo ambalo limetikisa nyoyo na vichwa vya
 waandaaji, wabunifu,wafanya biashara na watafuta vipaji vya kimataifa. Hii ni mara
ya kwanza kwa taifa letu kushiriki katika shughuli na wote wameguswa na
kupumbazwa na usanii wa hali ya juu ulioonyeshwa na wasanii watatu wa Kitanzania.
Barabara maarufu ya The Strand…
Ili kuunga mkono maendeleo ya Tanzania na Watanzania, Ubalozi wetu
 Uingereza na 
Bodi ya Utalii Tanzania, nao pia walichukua nafasi hii kuwasaidia
wananchi hawa kufanikisha mahitaji yao ya ushindani. Ubalozi umetoa Ukumbi wa
Nyumba Ya Tanzania ulioko 
Bond Street ili wasanii hao waweze kuonyesha nguo
 na sanaa zao kwa juma zima kama sheria za London Fashion Week zinavyoamuru.
 Vile vile Bodi ya Utalii ya Tanzania imesaidia katika mchango wa mali ghafi
zilizotumika katika shughuli hizi ili kuiuza Tanzania kimataifa.
Siku hii Tanzania ilikuwa moja ya nchi mbili tu za Kiafrika zilizochaguliwa na British
 Council na “London Fashion Week” kushiriki mashindano ya kutafuta vipaji chipukizi
 kwenye tasnia ya ubunifu wa mavazi na urembo. 
Watanzania Anna Lukindo,
Jacqueline Kibacha na Christine Mhando
ndio wasanii waliobeba
 bendera ya taifa letu na kutuwakilisha katika mashindano
haya ya kimataifa yanayofanyika kila mwaka kwa zaidi ya miaka 27 sasa.
Nje ya Jumba la Somerset- Samson Soboye (Mpangaji wa maonyesho),
 Jacqueline Kibacha
 (“Heart 365″), Mama Balozi Joyce Kallaghe, Anna Lukindo (“Anna Luks”)
 na Rose Kiondo 
 (Mratibu wa maonyesho)
Maonyesho ya London Fashion Week, bado yanaendelea jumba hil
 la 
Somerset  toka tarehe 14 hadi tarehe 28.
 Wiki hizi mbili nzima zitakutanisha kila mtu anaye husika
 na biashara ya mavazi na urembo. Magwiji na mapapa wa mitindo
, wabunifu, walimbwende,
watafuta vipaji, wafanya biashara,
  wazalishaji mali ghafi na wamiliki viwanda.
Wote hukutana katika maonyesho haya. Hapa si vipaji tu
vinavyojionyesha, 
bali pia watu wa biashara.

Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

No comments :


three columns

grids

health