Vijana wanaounda Ya Moto Bendi wameendelea kuwa moto wa kuotea mbali katika anga za kimatiafa ambapo mbali ya kufanya show za uhakika nchini Marekani,wamefanikiwa pia kuingia katika kuwana tuzo za Kora mwaka 2016.
Ya moto bendi ambao wanatamba na track zao mbalimbali kali zinazozidi kufanya poa katika redio na luninga nyingi hapa nchini,wameingia katika tuzo katika kipengele cha Most Promising Male Artist of the Year kupitia nyimbo yao ya ‘nitakupwelepweta’
Wasanii wengine watakao chuana na Ya Moto Band ni pamoja na Rekaardo Banks wa Nigeria,Chemi Boudraa wa Algeria,Numerica wa Cameroon,Odyai wa Madagascar na J Rio wa Gabon
No comments :