technology

business

LEO KATIKA HISTORIA-Jumanne, Disemba Mosi, 2015.Je Unajuwa Ukimwi Ulianzaje? Na mengine Mengi Yaliyofanyika Tarehe Kama Ya Leo.

Jumanne, Disemba Mosi, 2015

Leo ni Jumanne tarehe 19 Safar 1437 Hijria sawa na tarehe Mosi Disemba 2015.
Tarehe Mosi Disemba kila mwaka, nchi mbalimbali duniani huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Ukimwi.
 Ukimwi ni ugonjwa wa kuambukiza ambao unatokana na kurundikana kwa virusi vya HIV mwilini ambavyo huharibu mfumo wa ulinzi wa mwili na kutayarisha mazingira ya kushambuliwa na maradhi nyemelezi.
Ugonjwa huu ulibainika kwa mara ya kwanza kabisa nchini Marekani mwazoni mwa miaka ya 1980.
Wakati huo baadhi ya wanaume wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile huko New York na California waligundulika kuwa na kansa ambazo hazikukubali tiba ya aina yo yote. Japokuwa wakati huo, haikujulikana sababu ya maambukizi ya ghafla ya magonjwa hayo lakini tukio hilo limetambuliwa kuwa ndiyo mwanzo wa kujitokeza maradhi ya Ukimwi. Ugonjwa huo ambao haukuwa na jina ulienea kwa kasi kubwa katika kipindi cha mwaka mmoja na hatimaye mwaka 1982 ulipewa jina la Ukimwi.  
Miaka 189 iliyopita katika siku kama hii ya leo, muungano wa kihistoria wa nchi za Ulaya ulisambaratika baada ya kujiengua utawala wa Kikaitsar (Tsarist) wa Russia katika muungano huo. Muungano huo uliundwa kati ya tawala za Russia, Austria na ufalme wa Pros baada ya kuanguka kwa utawala wa Napoleon na kufanyika Congress ya Vienna, na kwa mujibu wake tawala hizo ziliafikiana kwamba nchi zilizo chini ya mamlaka ya muungano huo zifuate misingi ya dini ya Kikristo katika uhusiano wa kimataifa.
Na siku kama hii ya leo miaka 77 iliyopita Ayatullah Sayyid Hassan Mudarres, mwanazuoni mwa mapambano na mpigania ukombozi wa Kiirani aliuawa shahidi na vibaraka wa Reza Khan, mtawala dhalimu wa Iran wa wakati huo katika mji wa Kashmar kaskazini mashariki mwa Iran. Ayatullah Sayyid Hassan Mudarres aliamua kuanzisha mapambano dhidi ya utawala huo baada ya kujionea dhulma na ukandamizaji wa mtawala Reza Khan nchini Iran. Alifanya jitihada kubwa za kutekelezwa sheria za Kiislamu hapa nchini na kuiokoa Iran kutoka kwenye makucha na udhibiti wa wakoloni. Kwa msingi huo mtawala kibaraka wa wakati huo wa Iran, Reza Khan Pahlavi alimuona kuwa adui mkubwa na kuchukua uamuzi wa kumuua.
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

No comments :


three columns

grids

health