KWELI SI KWELI?
1-Mwanaume kwa kawaida anapomtamani mwanamke, hamtamani kama yeye kamili, bali humtamani vipande vipande. Hutamani mguu au kifua, midomo au nywele ama hata pua na pengine makalio. Mwanamke kwa mazingira fulani hufurahia jambo hilo, yaani kupendwa huko kwa viraka viraka. Lakini mwanamke hampendi mwanaume kwa viraka viraka bali kama alivyo.
2-Kwa kawaida mwanaume huweza kufurahia tendo la ndoa bila hata kumpenda mwanamke, lakini kwa mwanamke, hiyo ni tofauti, kwani hawezi kufurahia tendo la ndoa kama hajampenda mwanaume. Kwa mwanaume tendo la ndoa halihusiani kabisa na kupenda.
3-Mwanaume huweza kupata ashki hata kufikia kuamsha sehemu zake za siri kwa kutazama picha tu ya sehemu kama matiti, makalio na hata macho. Kwa hali hiyo, mwanaume hawezi kutofautisha kati ya kitu halisi na kitu bandia linapokuja suala la kujamiiana
. 4-Kwa wanaume kutongoza na kuwapata wanawake wazuri sana, huwa linaonekana kwao kama jambo la sifa na uthibitisho wa udume wao. Kwa hiyo baada ya kutongoza na kukubaliwa, huwa wamemaliza kazi. Suala siyo kutongoza kwa sababu mtu amependa, hapana,ni kwa sababu alitaka kuonesha na kujionyesha
SOURCE:JF
No comments :