Picha hii ambayo ameipost dada wa Kim anaeenda kwa jina la Khloe aliweka kwenye mtandao wake wa Instagram picha hii akimpongeza kim na kumpa pole kwa uchovu baada ya kujifungua.... Picha hii inayomwonesha Kim akiwa amelala pembezoni akiwa na mbwa wa Khloe dada wa kim.....!! Hii ndio picha ya kwanza kabisa kuonekana ya Kim Kardashian baada ya kujifungua wikii tatu nyuma mtoto wa kike..... Huku wengi wakiwa na shauku ya kuona picha itakayokuwa nzuri ya Kim na mtoto mwenyewe anaeitwa North West..... Ilisomekana comment ya shabiki mmoja kwenye post ya Khloe aliandika ''Tunahitaji kumwona mtoto jamanii kwanini mnatunyima raha,tunahitaji kukuona Kim kwanini wajificha? mashabiki zako tunakusubiri kwa hamu...!! Hiyo ni moja ya comment ya mashabiki wa Star huyo aliyeamua kutulia sasa na Mwanamuziki wa Hip-Hop Kanye west ambae ndie Baba Halisi wa Mtoto wake...!! Kwa sasa inasubiriwa kwa hamu picha ya mtoto wa star huyo kuonekana Japo magazeti mbalimbali yameanza kutuma ofa ya kununua haki miliki ya uchapishaji wa picha za mtoto North West....
Tusubiri tuone kama ni nani atashinda dili ilo au watafanya kama marafiki zao wa karibu Nikimaanisha Jay-z na Beyonce baada ya kumficha mtoto wao kwa kitambo waliweka picha za mtoto wa huyo Ivy Blue Carter kwenye mtandao wao wa Twitter na kuzima ndoto za majarida makubwa kununua na kuwa wamiliki wa Picha za Mtoto huyo...!! |
No comments :