Habari toka bongo movie nakuletea ww mpenzi wa filamu za kibongo,Ni mwanadada Nisha Bebe Pusi ameweza kufunguka kwenye one & one talk na detective wako wa Thisisdiamond kuhusiana na story behind kuwa kufanya vizuri kwenye movie na maendeleo ya kimaisha yanatokana na nguvu ya kigogo anaemuwezesha.... Nisha bebe amefunguka na kuongea haya ili kuwaweka wazi mashabiki zake Tanzania nzima alisema''Kwanza kabisa ieleweke mimi ni mjasiliamali na napenda kazi yangu sana,kwahyo hayo maneno yanayosemwa na kuandikwa mimi nashangaa,nimeanza zamani kwenye sanaa na kidogo nilichokuwa napata nakitunza hadi leo. Sasa mi nashangaa wakati mimi nipo busy naweka akili yangu chini kufikiria nini cha kufanya watanzania wakipokee vizuri nashangaa zinavuma story ooh mara naongwa mara kuna mtu anaesimama nyuma yangu basi wacha nkuambie anaesimama nyuma yangu ni Mungu pekee ndio anaeniwezesha kufika hadi hapa nimefika.....'' Nisha alizidi kufunguka kuhusu maswala ya kazi zake alikuwa na aya yakusema'' Napenda kuwaambia watanzania kuwa kuna baadhi ya wasanii wa kike wa Bongo movie wanafanya hila kulipa hata magazeti kunichafua mimi lakini mimi nasonga mbele kwa kuwa najua kabisa watanzania ndio wanaojua kazi yangu,naheshimu kazi yangu naeshimu watu wangu asa napoona nachafuliwa inakuwa inaniuma sana,kumbuka nami ni binadamu kwahyo yanapokuja kama haya yanaumiza lakini najikaza na kujipa moyo najua fika mwenyezi Mungu ndie anaenisimamia....'' Akijibu swali kuhusiana kuwa karibu na Jacquline wolper na mzee majuto kwenye movie alikuwa na aya yakusema ''Wakati naanza kuigiza nilikuwa na malengo nitimize ndoto zangu kuonekana kwenye Tv lakini muda ulivyozidi kwenda kipaji kikazidi nikasema kwanini nisifanye movie kuburudisha watanzania,ndio movie nilizocheza zikanitambulisha vyema kwa watanzania na kunikubali....Baada ya hapo nikaona kwanini nisifanye filamu kama kazi na kutengeneza hela kwa kuwa kabla ya hapo nilikuwa na biashara zangu zilizokuwa zinaniwezesha kukidhi mahitaji yangu......!! So kwenye sanaa nikakutana nao hao watu wawili na kuamua kufanya nao kazi nikawapa story kiukweli mzee majuto ni mzee mwenye busara sana na jacquline wolper ni mwanamke mwenye kiu ya mafanikio so tulivyokutana wote tuna kiu ya mafanikio tukajikuta tunaweza kufanya filamu ambayo nashukuru mungu watanzania wameikubali kwa moyo mmoja ambayo ni PUSI NA PAKU... Nimetoa movie nyingine ambayo kiukweli ni filamu iliyotumia muda mwingi wangu na wengine waliohusika akiwemo Hemed P.H.D,Mzee Majuto,Chuchu Hans na Jacquline Wolper.. Unaweza kuona hata Steps wameweza kuongea ndani ya mwezi huu movie yangu ndio imefanya vizuri ndani ya mwezi wa sita na watano,hii yote inatokana na kazi nzuri na kufanya kitu watanzania wanapenda.....
Alizidi kujibu swali lingine kuhusiana na kampuni yake ya Nisha's Film Production alikuwa na haya yakusema ''Chini ya Nisha's production tumeweza toa kazi kadhaa lakini mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu tunategemea kufanya kazi nyingi zaidi za kimataifa ikiwemo kufanya movie na movie star toka Nigeria na ghana lakini sintoweka wazi kwa sasa hadi muda utakapowadia''
Maoni kwa bongo movie.....''Napenda kuwasihi wadau wa Bongo movie kufatilia kazi hata za wasanii wachanga ambao bado hawajatoka kiubinafsi nina wasanii ambao chini ya Nisha's ntanza kuwachezesha wenye vipaji saawia kabisa so watanzania wakae mkao wa kula....!! Pia napenda kuwasihi wanawake waliokuwa kwenye Bongo movie kujituma na kuwa wajasiriamali wasiwe tegemezi za wanaume na kuacha fikra za kusubiria wapate wanaume wenye pesa kuwahudumia wageze mfano kama wangu kujituma ndio nguzo muhimu kwenye maisha huwezi fanikiwa kama huoneshi njaa ya mafanikio zaidi ya yote nawapa shukrani za dhati mwenyezi Mungu namashabiki zangu wanaopokea kazi zangu na kuwaahidi Inshallah kupokea kazi nzruri toka kwangu....
|
amependeza sana nampenda sana hy dada hasa uigizaji wake pale red cross matrida big up Mungu akujaalie ufike mbali
ReplyDelete