Ukilitaja jina hili Ulimwenguni basi akutakuwa na mtu anaefatilia maswala ya habari za dunia akose kumjua
binadamu huyu sana kwa upande wa Afrika ukimtaja huyu basi viongozi wengi wanamtambua,ila kwa huku afrika ya mashariki ukimtaja binadam huyu kwa viongozi wa kenya basi unaeza angushiwa varangati na ujute kwanini ulimuulizia,LUIS MORENO OCAMPO mwenye asili ya kiagentina ni mpelelezi na mfatiliaji mashitaka kwenye mahakama ya kivita dunia ambayo inajulikana kama HAGUE ambayo maka makuu yake yapo nchini Uholanzi...!! Aidha kwa upande wa afrika mashariki ewe kijana mwenzangu uliweza kumjua jamaa huyu kipindi yupo nchini kenya kufanya upepelelezi baada ya machafuko kutokea ya ghasia za uchaguzi wa mwaka 2008 nchini humo..... Ocampo aliezaliwa mnamo tareh 4.6.1952 nchini Argentina...... Ocampo anafahamika kama mpelelezi na mwendesha Mashtaka mkuu ndani ya The Hague... Tokea aanze kazi hiyo unaambiwa hajwahi kumfatilia mtu kiundani kutokana na maswala \ya kivita na akashindwa mfikisha kwenye mahakama hiyo na ushaidi tosha.. Mnamo mwaka 2004 Ocampo akiwa nchini Argentina alimfunga baba yake mzazi kwa kosa la kula rushwa nchini humo,hii ndio ilikuwa mojawapo ya chachu za yeye kupewa hata kazi kwenye mahakama hiyo kutokana na kufanya kazi kwa moyo mmoja...!!
Toka aingie madarakani yeye ameweza kuwatia nguvuni viongozi nguli wa Afrika mojawapo akiwa kama Charles Taylor aliekuwa kiongozi wa nchini Liberia na hadi anastaafu alikuwa akimuwinda Rais wa Somalia Ali Bashir japo akumtia nguvuni kila amtokeapo anakuwa sheria inambana kumkamatia nchini kwa mtu mwingine.....
Mwaka 2009 alikuwa sumu kali mithiri ya nyoka pale alipotua nchini Kenya kuanza upelelezi wa siku 72 hadi muda muafaka ulipofika na kuwataja waliochochea ghasia hizo nchini humo.......
Namuita ni adui namba moja kwa viongozi wa dunia kwa kuwa \ popote linapotokea tatizo au machafuko ya hali ya juu basi baada ya ghasia kutulia Ocampo lazima awasili mahala pale kujua ukweli wa mambo......
Ni hayo tu kwa leo mpenzi msomaji wa makala wa Thisisdiamond niandikie kwenye Email yangu Thisisdiamond89@gmail.com kuniambia unataka nikuandikie makala ya kiongozi,mwanamihcezo na taaluma tofauti tofauti... |
No comments :