technology

business

SALAMU ZA RAMBIRAMBI TOKA KWA WIZARA YA HABARI,VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO KUTOKANA NA KIFO CHA MANGWEHA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia 
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imepokea 
kwa mshituko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha msanii
 wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) Albert Mangweha, 
aliyefariki huko Afrika  Kusini katika hospitali ya St. Hellen akiwa
 katika shughuli za muziki, Jumanne  tarehe 28 Mei, 2013.

Kifo cha Albert Mangweha ni pigo kubwa kwa fani ya muziki 
hapa nchini, na pia kimataifa. Na kutokana na umahiri wake katika 
fani hiyo ya muziki wa kizazi kipya hususan aina yake ya uimbaji 
ya “Free Style” alikonga mioyo ya wapenzi wake hasa vijana 
ndani na nje ya nchi.

Albert Mangweha atakumbukwa na wasanii na wapenzi wa
 muziki  kwa kipaji na juhudi zake za kukuza muziki hapa nchini.
Serikali inawapa pole ndugu na jamaa wote  na kuwaomba 
wawe na uvumilivu na subira katika kipindi cha msiba.

Wito wa Serikali kwa wasanii na wananchi kwa ujumla ni 
kuendelea kumuenzi kwa  yale yote mazuri aliyoyafanya 
wakati wa uhai wake.
“Mwenyenzi Mungu ailaze roho ya Albert Mangweha 
mahala pema peponi.”

Imetolewa na
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo
Dkt Fenella Mukangara

Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

No comments :


three columns

grids

health