Edward Moringe Sokoine alizaliwa tarehe 1 Agosti 1938 alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania tarehe 13 Februari 1977 hadi tarehe 7 Novemba 1980 tena akawa Waziri mkuu toka tarehe 24 February hadi tarehe 12 Aprili 1984. Alikuwa ni mtu aliyepanda usawa kwa kila mtu aliamini kila mtu anaweza kuwa na maendeleo kama akijituma katika kilimo na sehemu alipo pamoja na kujitegemea akiwa ni wakala wa mabadiliko katika nchi, mtu asielaumu na mwaminifu. Alizaliwa Monduli Mkoani Arusha Tanzania, alipata elimu ya msingi na sekondari katika miji ya Monduli na Umbwe toka mwaka 1948 hadi 1958. Mwaka 1961 alijiunga na chama cha TANU baada ya kuchukua masomo katika Uongozi nchini Ujerumani 1962 hadi mwaka 1963. Aliporudi kutoka Ujerumani alikuwa Afisa Mtendaji wa Wilaya ya Masai, tena akachaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo la Masai. Mwaka 1967 alikuwa naibu waziri wa mawasiliano, usafiri na kazi. Hatua nyingine katika maisha yake alijitangaza mpaka kuwa Waziri Mkuu 1970. Mwaka 1972 aliamia kwenye Waziri wa usalama. Mwaka 1975 alichaguliwa kwenye Bunge tena wakati huu kupitia Monduli. Miaka miwili baadae akawa mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), 1977 alianza muhula wa kwanza ofisini akiwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania. Muhula huu ulidumu hadi 1981, baada ya kutulia kwa kipindi cha mwaka alikuwa tena Waziri Mkuu tena mwaka 1983, alikaa mwaka mmoja ofisini mpaka alipofariki Aprili 1984 kwa ajali ya gari. Kuna Chuo Morogoro Tanzania kinaitwa jina lake (Sokoine University Of Agriculture (SUA) kilianza mwaka 1984 kama chuo cha kilimo kinachotoa diploma katika kilimo. Chuo hicho kikaongezwa hadi kutoa mchepuo wa kilimo mwaka 1969 chini ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam. |
No comments :