Tamasha la Sauti za Busara linapokea maombi ya filamu za muziki wa kiafrika kwa kwa ratiba ya mwaka 2013. Toleo la kumi la tukio hili muhimu litachukua nafasi yake kuanzia tarehe 14-17 Februari ndani ya ukumbi wenye historia ndefu wa Ngome Kongwe, Zanzibar. Sauti a Busara inatafuta filamu tofauti kutoka pande zote za Afrika ambazo zitawaburudisha na wenyeji na wageni. Zinaweza kuwa video za muziki, rekodi za matamasha, makala za muziki au filamu za kiuchunguzi. Filamu bora zitachaguliwa na kuonyeshwa kubwa kabisa katika skrini ya tamasha. . - Fiamu inayoelezea muziki au mwanamuziki kutoka bara la Afrika na kwingineko.
- Filamu inayoelezea hazina na utofauti wa muziki wa Afrika masahriki na kwingineko.
- Filamu za muziki zitakazowavutia watazamaji wageni na wenyeji.
- Filamu yenye muonekano mzuri, ubora wa sauti na vilevile muziki uliotoka Afrika.
- Filamu mpya na sauti zisizowahi kusikika, na wasanii wapya
- Filamu za kigeni ni lazima ziwe na tafsiri ya kiingereza au kiswahili
Tamasha la Sauti za Busara ni tukio la kila mwaka ndani ya Afrika Mashariki na ambalo linajulikana kama “Tamasha rafiki ndani ya sayari”. Toleo lijalo la mwezi wa pili 2013 litakutanisha vikundi zaidi ya ishirini kutoka Afrika Mashariki na kwingineko, na wote hao nia yao moja kwa moja kutimiza matakwa ya sauti za busara kwa asilimia mia(100% live) |
No comments :