Kupitia kampuni yake ya Gorilla Films, Justin na mke wake Candice Campos ambaye pia ni producer wa video wamefanya kazi na wasanii wengi wa Tanzania hadi sasa, na kuna wengine wanaendelea kuwatafuta ili wafanye kazi.
Katika mahojiano Exclusive na Bongo5, Justin ametoa ushauri kwa ma-director wa Bongo kuhusu vitu vya kuzingatia ili kufanya video nzuri.
Justin Campos
Ameshauri wawe original, watazame video bora kutoka kwa waongozaji wengine duniani kwa lengo la kujifunza na kuvifanyia kazi kwenye mazingira ya nyumbani vile watakavyochukua.
“The best advice I can give is to kill the videos. Make them fantastic. Raise the bar, be original, watch the best videos in the world and adapt for the local market.” Alisema Justin.
BTS ya utengenezwaji wa ‘Don’t Bother ya Joh Makini
Kuhusu changamoto za video nyingi za wasanii wa Tanzania kukosa airplay kwenye vituo vya kimataifa, Justin amesema vituo hivyo hucheza video zenye nyimbo nzuri, msanii mzuri, pamoja na video nzuri hivyo ni jukumu la wasanii na waongozaji kuhakikisha wanaziongatia hayo wakati wa kuandaa video zao.
“Stations play videos that have a good song, good artist, good video” aliongeza Justin.
Swali lingine nililomuuliza ni kuhusu ni director gani wa Tanzania anayemfatilia kwenye kazi zake na anayemkubali zaidi, “Best director in TZ right now? Wow that’s not fair, right? Well I’d go with Hanscana, and I love his video for Chin Bees ft G-Nako “Pakaza” . alisema Justin
Justin na mkewe Candice Campos wakiwa na Hanscana
Wasanii wa Bongo ambao hadi sasa wamefanya video na Justin Campos ni Vanessa Mdee,
Navy Kenzo (Aika, Nahreel), Joh Makini, Ben Pol, Juma Jux, Shaa, G-Nako pamoja na Chege.
Justin na mkewe wakiwa na Navy Kenzo
Instagram : @paulchazzy
Whatsapp:
No comments :