Breaking News: Jose Mourinho atupiwa virago Chelsea
Jose Mourinho amefukuzwa kazi kama kocha wa Chelsea baada ya kunyukwa 2-1 na Leicester ikiwa ni muendelezo mbaya wa kikosi chake tangu msimu uanze.
Kocha huyo Mreno alikiongoza kikosi chake kunyakuwa taji la Ligi Kuu mwezi Mei, lakini kipigo cha Jumatatu kilikuwa cha tisa katika tangu msimu uanze, akiwa nafasi ya 16, ikiwa ni alama moja kushuka daraja.
Mourinho, ambaye alikuwa tayari kufanya mazungumzo kuhusiana na fedha wakati wa kuondoka kwake baada ya kipigo cha West Ham mwishoni mwa Oktoba, ameona msimu wake wa pili ukiishia ukingoni.
Lakini, akiwa tu amesaini mkataba mpya wa miaka mine msimu huu, huenda kukawa na mtafaruku wa malipo utakaotolewa na Chelsea.
Ni mara ya pili Mourinho kuondoka Chelsea ikiwa katika hali tete baada ya kufanya hivyo mara ya kwanza mwaka 2007.
No comments :