Hakika ukiwa na nyota ya Kung'aa basi daimanyota itawaka tu ili limeziilika kwa mchezaji mpira huyu aliestaafu kucheza soka mwishoni mwa msimu huu lakini juzi kati tu hivi amepokea dili nono na shavu la kutosha kutangaza
nguo za ndani za kampuni ya nguo kutoka sweden ijulikanayo duniani kama H&M... H&M kirefu ni Hennes & Mauritz wabunifu toka nchi za scandinavian wanaofanya shuguli zao nchini Uingereza katika kuboresha kazi zao na toleo lao jipya la nguo za ndani za kujistiri kwa wanaume wamempa dili ilo mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya uingereza David Beckham kutangaza kupitia matangazo ya picha na video nguo hizo uku siri ikifichuka kuwa kapteni huyo wa zamani wa Manchester United\ amelamba kitita cha Pound za kiingereza milion 9 kuziweka kibindoni, kisu kirefu sana kwa pesa ya kitanzania...!! Je kampuni hii ilishindwa kumtafuta mchezaji huyu kipindi anacheza soka kutangaza matoleo ya nyuma au? kwa upeo wa haraka nadhani ingekuwa bora zaidi au ni maswala ya mpunga ungekuwa mrefu sana tofauti na sasa...lakini sio ya msingi sana bahati inazidi kushamili kwa wanamichezo wa majuu hii pia inawapa changamoto wanamichezo wa Afrika kuzidi kufanya vizuri ili kucheza mpira kwa kiwango cha juu makampuni tofauti tofauti kuwatafuta kwa matangazo hata ubalozi wa muda mrefu...!! |
No comments :